dcsimg

Nge ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Akarabu (kundinyota)

Nge au akrabu (kutoka Kiarabu عقرب) ni arithropodi wa oda Scorpiones katika ngeli Arachnida. Spishi ndogo huitwa visusuli pia. Kama arakinida wote wana miguu minane. Pedipalpi zao ni kubwa na zina gando, na mkia ni mrefu na una msumari mkubwa mwishoni kwake. Kama kawaida kiwiliwili chao kina sehemu mbili: kefalotoraksi ( cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio lakini zimeungwa vipana, siyo kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija kama kwa buibui. Mgongo wa kefalotoraksi ni mgumu na kwa hivyo huitwa gamba (carapace). Nge wana macho 6-12, mawili juu ya gamba la kefalotoraksi na 2-5 kwa kila upande wa kichwa. Msumari wa nge hutumika kwa kudunga windo na kuingiza sumu ndani yake. Windo akiwa amekufa, kelisera (chelicerae) za nge zinakata vipande vidogo vinavyowekwa katika kishimo mbele ya mdomo. Maji ya umeng'enyaji yakamuliwa katika kishimo hiki na baada ya kumeng'enya chakula myeyuko ufyondwa. Nge hula arithropodi wengine na wale wakubwa hula mijusi na vipanya wadogo pia.

Picha

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Nge: Brief Summary ( Swahili )