Magonda ni mijusi-islam wa jenasi Trachylepis katika familia Scincidae. Spishi hizi ni mijusi-islam wa kimsingi wenye kope zinazoweza kusogea, matundu ya masikio yanayoonekana vizuri na mkia mrefu kuliko mwili. Miguu imekua vizuri na inabeba vidole vitano. Ngozi ni laini na inang'aa.
Mijusi hawa ni wafupi (sm 8-15) hadi warefu kiasi (sm 22-30); urefu mkubwa ni sm 35. Rangi yao ni kijivu au kahawia na pengine rangi nyingine kama nyekundu na buluu.
Huishi kati ya mawe, nyasi au matete au juu ya miti na vichaka. Chakula chao ni wadudu na invertebrata wengine.